Mwongozo wa Matumizi ya Ludewa Portal

Fahamu jinsi ya kutumia mfumo huu kurahisisha usimamizi wa taarifa na matokeo.

Matumizi ya Menyu ya Pembeni (Sidebar)

Menyu ya pembeni ndiyo njia kuu ya kufika kwenye kurasa mbalimbali za mfumo. Ukibonyeza kipengele chochote chenye mshale, kitashuka chini na kuonesha kurasa zake. Ukibonyeza ukurasa husika, utafunguka hapa katikati.

Vitufe Maalum Vinavyowaka

Ili kurahisisha matumizi ya mfumo na kuongeza ufanisi wa ki-UX, kuna vitufe maalum vinavyowaka-waka (brim-brim):
1. Kitufe cha Menyu ya Simu: Kiko juu kushoto (alama ya mistari mitatu ☰). Kinawaka ili kuwakumbusha watumiaji wa vifaa vidogo (simu) kubonyeza ili kuona na kufungua menyu ya pembeni (Sidebar) ambayo mara nyingi hujificha kwenye skrini ndogo.
2. Kitufe cha Mwongozo: Kiko kwenye dashibodi kuu ili kumsaidia mtumiaji kufika haraka kwenye maelekezo haya.

Usajili

Sehemu hii inatumika kusimamia usajili. Inajumuisha 'Maelekezo ya Mfumo' ya usajili pamoja na orodha ya 'Shule zilizokamilisha usajili'.

Ingawa eneo hili (Usajili), baadhi ya shule hazisajili wanafunzi wao kikamilifu. Tunasikitika sana, kwani wanasababisha zoezi zima la mchakato wa utoaji wa matokeo kuwa sio fanisi.

Results (Matokeo)

Hapa ndipo unapoangalia matokeo ya wanafunzi.

Unaweza kuangalia matokeo ya shule moja moja kwa kidato cha pili (F2) na kidato cha nne (F4).

Lakini pia unaweza kuangalia matokeo kwa ujumla (All Centers) kwa kidato cha pili (F2) na kidato cha nne (F4).

Performance (Ufaulu)

Tumia sehemu hii kupata mchanganuo wa ufaulu kwa wilaya nzima. Inajumuisha ufaulu kwa madaraja (Division Distribution) na orodha ya shule bora na duni kwa F2 na F4.

Ulinganifu wa Matokeo

Sehemu hii inakuwezesha kulinganisha matokeo ya mitihani tofauti au miaka tofauti ili kuona mabadiliko ya kitaaluma (kupanda au kushuka).

Report (Ripoti)

Hapa utapata ripoti za aina mbalimbali:
1. Ripoti ya Jumla (Overall Report): Hii inajumuisha mkusanyiko wa taarifa zote muhimu kuanzia utangulizi, orodha ya wanafunzi bora, na uchambuzi wa kina.
2. Ripoti za Mojamoja: Kama vile ripoti za mahudhurio (Attendance) kwa F2 na F4 zilizotenganishwa.

Ten Best (Kumi Bora)

Inaonesha wanafunzi 10 bora kiwilaya. Unaweza kuchuja kuona kumi bora kwa shule zote, shule za serikali pekee, au shule za serikali bila kujumuisha Ludewa Kwanza.

Kitufe cha Print

Unapokuwa umefungua ukurasa wowote wa matokeo au ripoti kutoka kwenye sidebar, kitufe cha "Fungua & Print" kitatokea chini upande wa kulia. Kikitumie kufungua ukurasa huo kwenye dirisha jipya ili uweze ku-print kirahisi.

Maelekezo Muhimu ya Ziada
Kwa maelekezo zaidi wasiliana nasi kwa simu: +255 765 883 980 au barua pepe: pmwasyika@gmail.com